Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 11, 2012

Ahmadinejad: Madola ya kikoloni yanataka kupora utajiri wa Mashariki ya Kati

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, madola ya kikoloni yanayotumia mabavu yanafanya njama za kupora utajiri wa nchi za Mashariki ya Kati. Dakta Ahmadinejad amesisitiza kwamba, Wamagharibi wakiongozwa na Marekani wamo mbioni kupora utajiri wa nchi za eneo hili. Amesema, madola ya kikoloni yamekuwa yakipeleka majeshi katika nchi mbalimbali na hivyo kujiandalia uwanja wa kupora mali na utajiri wa nchi hizo. Rais Ahmadinejad amezungumzia suala la miradi ya nyuklia ya Iran na kubainisha kwamba, nishati ya nyuklia ni haki ya wazi ya taifa la Iran na kwamba, taifa hili halitalegeza kamba hata kidogo katika kadhia hiyo. Aidha Rais Ahmadinejad amesema, tatizo la maadui ni kuwa, hawatambui adhama na uwezo wa taifa hili na wanadhani kwamba, kwa kutoa vitisho wanaweza kudhoofisha irada ya wananchi wa taifa hili. Dakta Ahmadinejad amekosoa pia siasa za kimabavu za maadui dhidi ya taifa hili na kuwaambia maadui hao kwamba, kulifanyia uadui taifa la Irani ni kwa madhara yao.

No comments: