Wanajeshi watiifu kwa jenerali Bosco Ntanganda wameunda kundi jipya la uasi huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kundi hilo la waasi limejiita M23 ili kuashiria mkataba wa amani wa Machi 2009 ambao uliwawezesha waasi wa CNDP kuingizwa katika jeshi la kitaifa Congo Kinshasa.
Aghalabu ya wanajeshi waliojiunga na kundi hilo jipya la waasi ni wapiganaji wa zamani wa CNDP. Kundi hilo jipya la waasi linaongozwa na kanali wa zamani jeshini. Kwa wiki moja sasa wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekuwa wakitekeleza oparesheni dhidi ya wanajeshi wanaomtii Ntanganda ambaye anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kwa tuhuma za jinai za kivita. Weledi wa mambo wanasema Ntanganda ameanzisha kundi la M23 kwa lengo la kuonyesha kuwa bado ana ushawishi mashariki mwa DRC hasa mkoa wa Kivu Kaskazini ili kwa njia hiyo ailazimishe serikali kufanya mazungumzo naye.Kundi hilo la waasi limejiita M23 ili kuashiria mkataba wa amani wa Machi 2009 ambao uliwawezesha waasi wa CNDP kuingizwa katika jeshi la kitaifa Congo Kinshasa.







No comments:
Post a Comment