Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 9, 2012

Ikhwanul Muslimin: Baraza la kijeshi lisiingilie uchaguzi Misri

Mjumbe wa Chama cha Uhuru na Uadilifu tawi la harakati ya Ikhwanul Muslimin nchini Misri, amelitaka Baraza la Kijeshi la Misri kutoingila uchaguzi wa rais nchini humo. Ahmed Jad ameyasema hayo hii leo katika mahojiano na televisheni ya Al Alam na kuongeza kuwa, baraza la kijeshi la nchi hiyo halipaswi kumsaidia mgombea yeyote katika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Ameongeza kwa kusema kuwa, wananchi wa Misri tayari wamekwisha chukua uamuzi wao wa nani watamchagua katika uchaguzi huo. Jad amelionya baraza la kijeshi la nchi hiyo kutomsaidia mgombea yeyote na kusema kuwa, kipindi cha utawala wa kijeshi kimefika mwisho. Ahmed Jad amesema, wananchi wa Misri wamechoka kutawaliwa kwa mtutu wa bunduki na wanajeshi nchini humo.

No comments: