Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 9, 2012

Iran yataka Israel ishinikizwe kuangamiza silaha zake za nyuklia

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa wito kwa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM kuushinikiza utawala haramu wa Israel uangamize silaha zake za nyuklia.
Akihutubu katika kikao cha NAM huko Sharm el Sheikh Misri, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kukataa utawala haramu wa Israel kujiunga na Mkataba wa Kuzuia Uenezwaji Silaha za Nyuklia NPT ni kizingiti kikuu katika kufikiwa pendekezo la Iran la Mashariki ya Kati isiyo na silaha za nyuklia.
Salehi amesema kuwa pendekezo la NAM la kuangamizwa silaha za nyuklia ifikapo mwaka 2025 linaweza kufikiwa tu iwapo nchi wanachama zitafuatilia kwa uzito suala hilo. Salehi aidha amezishukuru nchi za NAM kwa kuunga mkono shughuli za nyuklia za Iran zenye malengo ya amani na kusema sera hiyo inalinda haki za nchi zote kunufaika na teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani.

No comments: