Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, April 22, 2012

Free Press: White House inatoa mafunzo kwa makundi ya kigaidi

Gazeti la kila wiki linalochapishwa nchini Marekani lijulikanalo kwa jina la Free Press limeandika kuwa viongozi wa Ikulu ya Marekani White House wanatoa mafunzo ya ugaidi kwa watu wanaowaua kigaidi wasomi wa Kiirani.

Gazeti la kila wiki la American Free Press limeandika leo kuwa, licha ya kwamba Rais Barack Obama wa Marekani anazungumzia udharura wa kutumika udiplomasia na kufanya mazungumzo na Iran, lakini wakati huo huo viongozi wa White House wanaendesha siasa za kutoa mafunzo kwa makundi ya kigaidi kwa lengo la kuwauwa makamanda wa kijeshi na wasomi wa Kiirani.
Gazeti hilo la kila wiki la Free Press linalochapishwa huko Marekani limeendelea kuandika kuwa, Rais Obama anaendesha siasa ambazo zilikuwa zikiendeshwa pia na Rais wa zamani wa nchi hiyo George W. Bush na makamu wake Dicky Cheney.
Mwandishi wa gazeti hilo anayejulikana kwa jina la Simon Harsh anasema kuwa, serikali iliyopita ya Marekani mwaka 2003 iliruhusu kupewa mafunzo wanachama wa kundi la kigaidi la Munafiqin la MKO huko katika jangwa la Nevada nchini Marekani.
Kundi la Munafiqin limehusika katika jinai chungu nzima huko Iraq na hapa Iran zikiwemo za kuwauwa raia wasio na hatia wa nchi mbili hizi.

No comments: