Mufti Mkuu wa Syria amesisitizia udharura wa kujiepusha wananchi wa nchi hiyo na mifarakano hasa katika mazingira nyeti ya sasa ya mgogoro wa nchi hiyo. Mufti Mkuu Sheikh Ahmad Badreddin Hassoun amewataka wananchi wa nchi hiyo kudumisha umoja na mshikamano baina yao ili waweze kukabiliana na njama za maadui zinazoiandama nchi hiyo. Mufti wa Syria amesema kwamba, mifarakano nchini Syria sio tu ni kwa manufaa ya maadui nchini humo bali kwa eneo lote la Mashariki ya Kati.
Sheikh Ahmad Badreddin Hassoun ameongeza kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel, Marekani na waitifaki wao wa Magharibi wamekuwa wakifanya njama za kuzusha mifarakano katika Mashariki ya Kati na wamekuwa wakitumia nyenzo mbalimbali kwa ajili ya kufikia lengo hili.







No comments:
Post a Comment