Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 4, 2012

Kikwete atangaza rasmi Baraza jipya la Mawaziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ameweka hadharini orodha ya majina ya Mawaziri pamoja na manaibu waziri, Baraza hilo limetangazwa leo hii katika Ikulu yake jijini Dar es Salaam. katika majina ya mawiziri ameongeza sura mpya huku Mbunge aliyemteu leo Bi Saada Mkuya Salum kuwa naibu waziri fedha na kufanya wizara ya fedha kuwa na manaibu waziri wawili(wanawake).

Rais Kikwete amebadilisha baadhi ya Mawaziri ambao ndio gumzo nchi kutokana na skendo zao mbalimbali huku aliyekuwa Waziri wa nishati na madini, Waziri wa fedha wakienguliwa madaraka yao na kukabidhiwa wengine.

No comments: