Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, June 20, 2013

ICC: Kesi ya rais wa Kenya kuanza mwezi Novemba

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetangaza kuwa, tarehe ya kuanza kesi dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta imesukumwa mbele hadi Novemba 12, mwaka huu.  
Hatua hiyo inakusudiwa kuwawezesha mawakili wake kujiandaa barabara.Awali, ICC ilikuwa imepanga kesi hiyo ianze kusikizwa Julai 9, ingawa Bw Kenyatta, kupitia wakili wake, aliomba kuongezewa muda wa kujitayarisha kutokana na kuchelewa kwa upande wa mashtaka kueleza ushahidi unaotumiwa dhidi yake.
Taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo imesema tarehe hiyo mpya imezingatia ombi la mtuhumiwa pamoja na masuala mengine muhimu.
Rais wa Kenya anakabiliwa na makosa matano ya jinai dhidi ya binadamu ambayo ni mauaji, uhamishaji wa watu kwa lazima, ubakaji, dhulma na vitendo vya kinyama wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.

No comments: