Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 9, 2012

Msafara wa waangalizi wa Kimataifa wakumbwa na mlipuko wa bomu Syria

Mlipuko mmoja umetokea katika msafara wa waangalizi wa Kimataifa huko kusini mwa Syria na kupelekea watu 6 kujeruhiwa. Mlipuko huo umetokea leo asubuhi ukiulenga msafara wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa ulipokuwa ukipita katika eneo la Dara'a huko kusini mwa nchi hiyo na kuwajeruhi wanajeshi sita wa Syria akiwemo kamanda mmoja, ambao walikuwa wanausindikiza msfara huo. Jenarali Robert Mood Mkuu wa Ujumbe wa Wasimamizi wa Kimataifa nchini humo ni miongoni mwa waliokuwa katika msafara huo. Hata hivyo hakuna yeyote katika timu hiyo ya waangalizi aliyejeruhiwa.
Jumla ya waangalizi wa Kimataifa wapatao 60 wako nchini Syria na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka na kufikia 300 katika wiki zijazo.

No comments: