Thabo Mbeki, mpatanishi wa Umoja wa Afrika katika mazungumzo ya kitaifa
ya Sudan leo amewasili mjini Khartoum, kwa lengo la kufatilia mwenendo
wa mazungumzo hayo yaliyopendekezwa na Rais Omar al Bashir wa nchi hiyo.
Mbeki anatazamiwa kuzungumza na kubadilishana mawazo kuhusu mazungumzo
ya kitaifa na viongozi wa vyama na makundi ya upinzani wakiwemo wa chama
cha Umma, chama cha Kongresi ya wananchi, chama cha Muungano wa
Kidemokrasia na chama cha Mageuzi Sasa.
Mahmoud Kan, mwakilishi wa Umoja
wa Afrika nchini Sudan amesema, kutokana na ombi la serikali ya
Khartoum na pande nyengine nchini humo, Mbeki atajaribu kuzikurubisha
pande husika katika mazungumzo hayo ya kitaifa na kujenga hali ya
kuaminiana baina yao pasina kuingilia mchakato wa mazungumzo hayo.
Akiashiria mazungumzo ya Addis Ababa baina ya serikali ya Sudan na
makundi ya waasi, mwakilishi wa AU nchini humo amesema mazungumzo hayo
yataanza tena katika wiki ya mwisho ya mwezi huu wa Mei. Mnamo mwezi
Januari mwaka huu Rais Omar al Bashir wa Sudan alitangaza mpango wa
mazungumzo ya kitaifa kati ya serikali na makundi na vyama vya siasa
pamoja na waasi wanaotumia silaha kama njia ya kumaliza mgogoro
ulioikumba nchi hiyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment