Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, December 28, 2013

Wanajeshi wanane wa Chad wauawa J/Afrika ya Kati

Wanajeshi wanane kutoka Chad wanaolinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wameuawa nchini humo. Msemaji wa vikosi vya kulinda amani vya Kiafrika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati MISCA amesema kuwa, wanajeshi hao wameuawa kwenye mapigano yaliyojiri Bangui, mji mkuu wa nchi hiyo. Hata hivyo, msemaji huyo wa MISCA hakutoa maelezo zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Hivi karibuni, vikosi vya MISCA vilipanga mkakati wa kuwaondoa wanajeshi wa Chad katika mji mkuu wa Bangui na kuwapeleka kaskazini mwa nchi hiyo kwa lengo la kulinda amani. Inadaiwa kuwa, Chad inawaunga mkono wafuasi wa waasi wa zamani wa Muungano wa Seleka ambao ni Waislamu. Inafaa kuashiria hapa kuwa, jana wafuasi wa kundi la Anti Balaka walitekeleza mauaji ya kinyama kwenye Masjidul Nour mjini Bangui kwa kuwauwa Waislamu wasiopungua 23 wakiwemo wanawake na watoto. Waislamu hao walikimbilia Msikitini ili kupata hifadhi, lakini hawakusalimika kwani walivamiwa na Wakristo wa kundi la Anti Balaka na kuuawa kwa kukatwakatwa kwa mapanga na mundu.

No comments: