Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, December 28, 2013

Miili 44 yapatikana baada ya mapigano CAR

Wahudumu wa shirika la utoaji misaada la Msalaba Mwekundu wamekusanya miili 44 katika barabara za mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Bangui, ikiwa ni baada ya mapigano makali yaliyojiri kwa siku mbili zilizopita.  Georgios Georgantas, mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu amesema, kuna uwezekano miili hiyo ni sehemu tu ya idadi kubwa ya watu waliouawa katika mapigano yanayoendelea kwenye mji huo. Waasi wa zamani wa Seleka ambao wengi wao ni Waislamu wamekuwa wakipambana na wanamgambo wa Kikiristo kwa siku kadhaa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Hayo yanajiri huku askari 6 wa kulinda amani wa Chad wakiuawa pia katika nchi hiyo, na kugunduliwa pia kaburi la umati lililokuwa na miili ya watu 30 karibu na kituo kimoja cha jeshi.
Wakati huo huo viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wameutaka Umoja wa Mataifa kupeleka askari wa kulinda amani nchini humo ili kuhitimisha mapigano.

No comments: