Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, June 7, 2013

Uchaguzi wa Madagascar kufanyika mwezi Agosti

Baraza la Mawaziri nchini Madagascar, limekubaliana kusogeza mbele uchaguzi wa rais wa nchi hiyo, hadi mwezi Agosti mwaka huu. Waziri wa Mawasiliano wa Madagascar Harry Laurent Rahajason ametangaza leo kuwa, Baraza la Mawaziri limekubaliana kuwa, uchaguzi wa rais uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 24 Julai, utafanyika tarehe 23 mwezi Agosti mwaka huu. Kiongozi huyo wa Madagascar amefafanua kuwa, ili kuiepusha nchi hiyo na mgogoro wa kisiasa unaoikabili hivi sasa Madagascar, lazima tarehe hiyo iungwe mkono pia na Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo na Umoja wa Mataifa. Hatua hiyo inatajwa kuwa ni kuitikia ombi la mahakama maalumu ya uchaguzi nchini humo CES ambayo tarehe 28 mwezi jana, ilitaka kufanyiwa uchunguzi wa haraka nukta mbili za kusimamishwa msaada wa fedha za bajeti ya uchaguzi na kadhia ya kupingwa na jumuiya ya kimataifa, ugombea wa wagombea watatu wa nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo hapo jana mahakama ya uchaguzi ya nchi hiyo, iliidhinisha wagombea hao watatu ambao ni pamoja na Rais Andry Rajoelina, Lalao Ravalomanana, mke wa Marc Ravolamanana rais wa zamani wa Madagascar na Didier Ratsiraka dikteta wa zamani wa nchi hiyo kushiriki katika uchaguzi huo wa rais nchini humo.

No comments: