Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, July 2, 2013

Saudia: Magaidi wa Syria wapewe silaha

Serikali ya Saudi Arabia imeendeleza chuki na uadui wake dhidi ya serikali ya Syria, baada ya kuutaka Umoja wa Ulaya kutekeleza kivitendo uamuzi wake wa kuyaondolea vikwazo makundi ya kigaidi nchini Syria.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Saudi Arabia Saud al Faisal amesisitiza kuwa, Umoja wa Ulaya unapasa kutekeleza kivitendo maamuzi iliyoyachukua ya kuyaondolea vikwazo vya silaha makundi ya kigaidi yanayopambana na majeshi ya Syria.
Al Faisal amesisitiza pia ulazima wa kuchukuliwa misimamo ya kimataifa ya kukabiliana na waungaji mkono wa serikali ya Syria na kusema kuwa, baadhi ya duru za kimataifa zinatoa visingizio juu ya uungaji mkono wao kwa makundi ya kigaidi nchini Syria na kubainisha kuwa tatizo kuu ni hitilafu zilizopo kati ya wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na mgogoro wa Syria.
Serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria imekuwa ikikabiliwa na machafuko kutokana na misimamo yake madhubuti ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kuwa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

No comments: