Waziri mmoja wa Syria amesema kuwa ugaidi wa zaidi ya miaka
miwili unaofadhiliwa na nchi za Magharibi huko Syria umeharibu majengo
ya serikali yasiyopungua 9000 na kuisababishia setka ya umma hasara ya
dola bilioni 15. Omar Al Ibrahim Ghalaounji Waziri wa Serikali za Mitaa
wa Syria amesema hasara za mabilioni hayo ya dola zilisababishwa na
magaidi kati ya mwezi Machi mwaka juzi na Machi mwaka huu.
Omar al Ghalaounji amesema hasara zote hizo ni matokeo ya
mashambulizi ya kigaidi dhidi ya majengo ya serikali na miundo mbinu ya
Syria.
Hii ni katika hali ambayo Abdullah al Dardari Waziri wa zamani wa
Mipango wa Syria pia hivi karibuni alieleza kuwa mgogoro wa nchi hiyo
umeisababishia nchi hiyo hasara ya kati ya dola bilioni 60 hadi 80.







No comments:
Post a Comment