Rais Bashar al Assad wa Syria amepiga marufuku utumiwaji watoto
kwenye operesheni za kijeshi na kusisitiza kuwa watakaopatikana na hatia
ya kuwatumia watoto hao watakabiliwa na adhabu kali ya kifungo jela.
Rais Assad ameongeza kuwa, mtu yeyote atakayethubutu kuwashirikisha
vijana walio na umri wa chini ya miaka 18 kwenye oparesheni za kijeshi
na masuala yanayofungamana nayo kama kubeba silaha, zana za kijeshi na
kutega mada za milipuko kwenye vituo vya ukaguzi na maeneo mengineyo
watakabiliwa na kifungo cha kuanzia mwaka mmoja hadi 10 jela na kulipa
faini ya lira milioni tatu.
Rais wa Syria ameongeza kuwa, adhabu ya kifungo cha maisha itatolewa
kwa watu ambao watapatikana na hatia ya kuwalazimisha watoto kubeba mada
za milipuko na iwapo watoto hao watauawa, basi wahusika watakabiliwa
na adhabu ya kifo.







No comments:
Post a Comment