Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, July 2, 2013

Operesheni ya UN ya kulinda amani Mali yaanza

Umoja wa Mataifa umeanza operesheni ya kulinda amani nchini Mali kwa kuanza kusimamia askari 6,000 wa nchi za Afrika magharibi ambao tayari wapo nchini humo. 
Hafla za kuanza operesheni hizo zimefanyika leo mjini Bamako. Imepangwa kuwa hadi ifikapo mwezi Disemba kikosi cha kulinda amani cha UN nchini Mali kitakamilika kwa kuwa na askari 12,640. Kikosi hicho kipya kinaaza shughuli zake ikiwa miezi kadhaa imepita tangu Ufaransa iliyoishambulia kijeshi nchi hiyo kwa kisingizio cha kupambana na waasi, ianze kuondoa wanajeshi wake nchini Mali.
Kikosi hicho kinachojulikana kama MINUSMA kitaongozwa na jenerali Jean-Bosco Mazura wa Rwanda ambaye alikuwa afisa msaidizi wa kikosi cha askari wa Afrika wa kusimamia amani katika jimbo la Magharibi mwa Sudan la Darfur.
Operesheni hizo zina lengo la kuimarisha amani katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwezi huu.

No comments: