Habari kutoka Cairo mji mkuu wa Misri zinasema kuwa mawaziri 4
wamejiuzulu leo Jumatatu na kutangaza kwamba wanawaunga mkono wananchi
wanaopinga utawala wa Rais Mohammad Mursi.
Mawaziri walioachia ngazi ni Hisham Zaazou (Utalii), Atef Helmi
(Teknolojia ya Habari na Mawasiliano), Hatem Bagato (Sheria na Masuala
ya Bunge) na Khaled Abdul-Aal (Mazingira). Habari zaidi zinasema
mawaziri hao wamekabidhi barua zao za kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, Hisham
Qandil. Wachambuzi wengi wanakubaliana kuwa hatua hiyo ni pigo kwa
serikali ya Rais Mohammad Mursi hususan wakati huu ambapo kiongozi huyo
anakabiliwa na mashinikizo ya umma ya kujiuzulu.
Huku hayo yakijiri, maandamano yanaendelea katika miji mbalimbali ya
Misri. Waandamanaji katika miji ya Alexandria, Suez na Port Said
wamevamia na kuchoma moto ofisi za chama cha JEP cha Rais Mursi.
Wapinzani wamesisitiza kwamba wataendelea na maandamano hadi pale Dkt.
Mursi atakapojiuzulu.
Wakati huo huo jeshi la Misri limewapatia wanasiasa wa nchi hiyo
mudaa wa masaa 48 kutatua mgogoro wa sasa wa nchi hiyo la sivyo
wataingilia kati ya kuamua mustakbali wa nchi hiyo.







No comments:
Post a Comment