Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, July 2, 2013

"Marekani iweke wazi msimamo kuhusu Geneva 2"

Russia imeitaka Marekani kuweka wazi msimamo wake kuhusu mkutano wa Geneva 2 utakaofanyika kwa lengo la kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Syria.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov ambaye leo anaelekea Brunei ili kushiriki katika kikao cha jumuiya ya ASEAN, amesema kuwa Marekani inapaswa kutoa maelezo kuhusiana na kikoa hicho ambacho kufanyika kwake kulipendekezwa na Moscow pamoja na Washington kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Syria.
Lavrov ameongeza kwamba yeye na mwenzake wa Marekani walikubaliana kuishawishi serikali ya Syria na waasi wanaofadhiliwa na nchi za kigeni kutafuta suluhisho la kisiasa la mgogoro huo.
Katika upande mwingine serikali ya Syria imetangaza kuwa, mapigano ya miaka mwili yaliyosababishwa na magaidi wanaofadhiliwa na nchi za kigeni yameharibu majengo 9,000 na kuleta hasara ya dola bilioni 15.

No comments: