Rais Barack Obama wa Marekani amezitaka nchi zinazopakana na Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo kuacha mara moja uungaji mkono wao kwa makundi
ya waasi nchini humo.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Ikulu mjini Dar es
Salaam akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais
Obama pia amemtaka Rais Joseph Kabila wa Kongo kupanga mikakati ya
haraka ya kulikarabati na kulijenga upya jeshi la nchi hiyo. Rais wa
Marekani ameongeza kuwa, wananchi wa Kongo wanahitaji kupewa fursa,
kwani mapigano ya miaka kadhaa nchini humo yamewanyima fursa ya kupiga
hatua za kimaendeleo.
Obama amesema kuwa, makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwezi
Februari mwaka huu yenye lengo la kurejesha amani na utulivu mashariki
mwa Kongo hayapaswi kubaki kwenye makaratasi bali yanabidi kufanyiwa
kazi. Rais Barack Obama wa Marekani aliwasili Tanzania jana alasiri kwa
ziara ya siku mbili, baada ya kuzitembelea nchi za Senegal na Afrika
Kusini.







No comments:
Post a Comment