Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Bi. Catherine Ashton leo
Jumatatu amemtaka Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry kutoa
maelezo kuhusu tuhuma zilizotolewa na afisa wa zamani wa CIA kwamba
vyombo vya usalama vya nchi yake vimekuwa vikiwafanyia ujasusi
wanadiplomasia wa EU.
Duru za habari zinaarifu kwamba, Kerry alipatwa na kigugumizi
alipotakiwa kutoa maelezo hayo ambapo amesema hajui lolote kuhusiana na
tuhuma hizo.
Waziri John Kerry amesema atatoa taarifa kamili baada ya
kujua mbivu na mbichi kuhusu kadhia hiyo.
Afisa wa zamani wa CIA, Edward Snowden ameliambia jarida la Der
Spiegel la Ujerumani kwamba, Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani
(NSA) limekuwa likiwachunguza kwa siri na kuwafanyia ujasusi
wanadiplomasia wa EU katika miji ya Washington, New York na Brussels.
Jambo hilo limelaaniwa vikali na maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa
Ulaya.







No comments:
Post a Comment