Mahakama ya Viwanda nchini Kenya imetoa agizo linalowataka walimu
wa shule za umma walioko mgomoni kusitisha mgomo huo na kuripoti katika
maeneo yao ya kazi kesho Jumanne saa mbili asubuhi.
Agizo hilo la mahakama ya viwanda limetolewa baada ya serikali kudai
kwamba mgomo wa walimu ulioanza Jumanne iliyopita si halali. Mahakama
hiyo aidha imeitaka serikali kubuni kamati ya maridhiano itakayoongoza
mazungumzo kati yake na chama cha walimu. Hata hivyo, mwenyekiti taifa
wa chama cha walimu nchini humo KNUT, Bw. Wilson Sossion amesema walimu
hawatotii agizo hilo na kusisitiza kwamba mgomo utaendelea.
Weledi wa masuala ya sheria wameonya kwamba huenda viongozi KNUT
wakachukuliwa hatua za kisheria iwapo wataendelea kukaidi agizo la
mahakama. Walimu wanadai marupurupu yao kulingana na mkataba wa mwaka
1997 waliotiliana saini na serikali.







No comments:
Post a Comment