Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, May 10, 2012

Uganda yasema huenda ikalifukuza shirika la Oxfam katika nchi hiyo

Uganda imetishia kulifukuza shirika la misaada la Oxfam baada ya shirika hilo la Uingereza kuituhumu serikali ya Kampala kwamba ilishiriki katika vurugu za uporaji ardhi ili kujipatia faida ya kibishara.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uganda imeliambia shirika la Oxfam na la Uganda Land Alliance kwamba yatapoteza vibali vyao vya kuendesha shughuli nchini humo kama hayatatupilia mbali madai hayo na kuomba msamaha kuhusiana na tuhuma kwamba zaidi ya watu laki mbili waliondolewa katika ardhi zao ili kutengeneza njia kwa ajili ya shirika moja la misitu la kimataifa.
Wizara hiyo imesema kwamba, madai hayo yanamlenga Rais Museveni na kumjengea kiongozi huyo jina baya kwa namna ambayo haikubaliki katika sheria za kimataifa.
Serikali ya Uganda inasema kuwa watu hao waliondolewa katika eneo hilo kwa sababu walikuwa wakiharibu na kuhujumu hifadhi ya taifa ya misitu.

No comments: