Wanajeshi waliompindua rais was Mali aliyeondoka mamlakani, Amadou Toumani Toure, wametangaza kuwa wamedhibiti kambi kuu ya kijeshi katika mji mkuu wa Mali, Bamako.
Tangazo hilo limetolea baada ya makabiliano na wanajeshi waliotaka kumrejesha mamlakani kiongozi huyo wa zamani.Wanajeshi hao ambao hadi sasa wangali wanadumisha amani mjini Bamako, walikabiliana na mahasimu wao wanaodai wanataka kumrejesha mamlakani Bwana Toure, kwa siku mbili mfululizo.






