Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, February 10, 2015

Wanamgambo wadai kuuzingira mji muhimu Ukraine

Wapiganaji wa makundi yanayopigania kujitenga maeneo ya mashariki mwa Ukraine wamedai kuuzingira mji wa kistratejia wa Debaltseve. Wapiganaji hao pia wamesema mbali na mji huo, pia wamewazingira wanajeshi zaidi ya 1000 wa Ukraine mjini hapo. Serikali ya Kiev imekanusha madai hayo na kusema mapigano bado yanaendelea. Mji huo wa Debaltseve una umuhimu mkubwa kwani ndio unaotumiwa na wanajeshi wa serikali ya Ukraine kupitishia vifaa muhimu kutoka Kiev.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, kesho marais wa Russia, Ukraine, Ufaransa na Kansela wa Ujerumani wanatarajiwa kukutana mjini Minsk nchini Belarus ili kujadili namna ya kuhitimisha mapigano mashariki mwa Ukraine. Nchi za Ulaya zinaituhumu Russia kuwa inawaunga mkono wanamgambo wanaopigania kujitenga na Ukraine lakini Moscow imekuwa ikikanusha vikali madai hayo na kuzilaumu nchi za Ulaya kuwa ndizo zilizopelekea kuzuka machafuko hayo baada ya kuunga mkono mapinduzi yaliyomuondoa madarakani raia aliyechaguliwa kidemokrasi nchini humo.

No comments: