Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, February 10, 2015

"Sitoshirikiana na US kwani inaunga mkono magaidi"

Rais Bashar al-Assad wa Syria amekataa kushirikiana na muungano wa Marekani dhidi ya Daesh, kutokana na muungano huo kuendelea kuyaunga mkono magenge hayo yanayotenda jinai. Amesema kuwa, serikali ya Damascus haiwezi kushirikiana na nchi hizo ingawa pia amesema kuwa inaweza kushirikiana na nchi nyengine.
Rais al-Assad ameyasema hayo katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa na televisheni ya BBC na kusisitiza kuwa, Syria imeshapokea ujumbe kadhaa kutoka muungano huo unaoongozwa na Marekani ukiitaka nchi hiyo kushirikiana na Washington lakini mara zote Damascus imekuwa ikikataa ujumbe huo. Amesema na hapa ninamnukuu: “Tunapinga kuungana na muungano huo kama ambavyo pia hatupendelei kufanya hivyo. Na sababu iko wazi nayo ni kwamba, hatuwezi kuungana na nchi ambazo zinaunga mkono ugaidi. Wanakanyaga kanuni wazi wazi, hasa inapokuwa kadhia ni ya Syria.” Mwisho wa kunukuu. Akielezea madai ya Marekani ya kuwapatia mafunzo ya kijeshi watenda jinai ikidai kuwa ni wapinzani wenye misimamo ya wastani, amesisitiza kuwa, madai hayo hayana ukweli wowote na ni ndoto kwa Damascus kukubali kushiriki kwenye mungano wa unaoongozwa na Marekani.  Aidha Rais Bashar al-Assad amesema kuwa, aidolojia ya kundi la kitakfiri la Daesh na makundi mengine kama hilo, ni aidolojia ile ile ya Uwahabi unaoungwa mkono na ukoo wa Aal-Saudi wa nchini Saudia.

No comments: