Takriban wahajiri haramu 29 wa Kiafrika wamepoteza maisha katika kisiwa
cha Lampedusa karibu na Italia. Habari zinasema kuwa wahajiri
wasiopungua 100 wamezuiwa kuingia Ulaya na wanajeshi wa baharini wa
Italia ambapo 29 kati yao wamefariki dunia baada ya kupigwa na baridi
kali. Baadhi ya wahajiri hao wanaendelea kupata matibabu katika
hospitali moja kwenye kisiwa cha Sicily nje kidogo ya Lampedusa.
Hii si
mara ya kwanza kwa wahajiri haramu wa Kiafrika kupoteza maisha wakiwa
safarini kuelekea Italia. Mwaka uliopita pekee, zaidi ya wahajiri 3200
walipoteza maisha kwenye safari za aina hiyo. Mwaka 2013 wahajiri wa
Kiafrika wasiopungua 360 walipoteza maisha baada ya meli yao kuzama
katika kisiwa cha Lampedusa. Wengi wa wahajiri hao haramu huwa ni kutoka
nchi zilizoko chini ya jangwa la Sahara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment