Maeneo kadhaa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yameshuhudia mapigano
kati ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na muungano wa
zamani wa waasi wa Seleka. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na askari
hao wa Umoja wa Mataifa, mapigano hayo yalijiri katika eneo la Bria,
katikati mwa nchi hiyo.
Inaelezwa kuwa, mapigano hayo makali kati ya
pande mbili yaliibuka baada ya askari wa Umoja wa Mataifa kwa
kushirikiana na askari wa Ufaransa, kutaka kuwapokonya waasi hao wa
Seleka majengo ya serikali ambayo wamekuwa wanadhibiti kwa muda mrefu
sasa, suala ambalo limezusha mapigano makali. Hata hivyo taarifa kamili
ya idadi ya watu waliouawa au kujeruhiwa bado haijatolewa. Mbali na
waasi wa Seleka, askari hao wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa,
wamekuwa wakikabiliwa pia na mashambulizi kutoka kwa wanamgambo wa kundi
la kigaidi la Anti-Balaka suala ambalo wiki kadhaa zilizopita,
lilipelekea askari kadhaa wa umoja huo kuuawa na wengine wengi
kujeruhiwa. Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika mapigano makali
ya kikaumu hapo mwaka 2013 na kupelekea maelfu ya watu kuuawa, wengi
wao wakiwa ni Waislamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment