Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, February 10, 2015

Iran kuzindua meli mpya ya kivita ya ‘Damavand’

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeli Habibullah Sayyari amesema kuwa, karibuni hivi jeshi la wanamaji la Iran litazindua meli ya kisasa aina ya Damavand ambayo imeundwa na wataalamu wa hapa nchini. Akiashiria uwezo wa jeshi la Iran katika kujibu chokochoko zozote za adui katika sherehe za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran, Kamanda Habibullah Sayyari amesema kuwa, hii leo taifa la Iran linajivunia juhudi za wasomi na vijana wake ambao wameweza kuzalisha aina mbalimbali ya silaha na zana za kisasa kabisa kwa kiwango cha kimataifa.
Ameyataja mafanikio hayo kuwa ni mwiba kwenye macho ya maadui wasiolitakia mema taifa na watu wa Iran ya Kiislamu. Aidha ameelezea matatizo yaliyokuwa yakilikabili jeshi la Iran katika kipindi cha utawala wa Shah kutokana na kufuata kibubusa siasa za Marekani na kuongeza kuwa, wakati ule maamuzi na mipango yote yaliyokuwa yakihusu zana, silaha, mazoezi ya kijeshi na mambo mengine yalikuwa yakichukuliwa na Washington bila ya kuwahusisha wataalamu wa Iran, suala ambalo liliifanya Iran kubakia tegemezi wakati wote. Amesema kuwa, tangu mwanzoni mwa vita vya kulazimishwa vya miaka minane, Imam Khomein (MA) alitoa somo kwa jeshi la Iran kujiamini, jambo lililoifanya Iran iweze kusimama kidete dhidi ya mabeberu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

No comments: