Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, June 3, 2014

Watu 120 wuawa katika mapigano nchini Yemen

Naibu Mkuu wa Mkoa wa Imran nchini Yemen amesema kuwa watu zaidi ya 100 wameuawa katika mapigano yaliyozuka baina ya jeshi la serikali na wapiganaji wa al-Huthi kaskazini mwa nchi hiyo. Ahmad al-bakri, amesema kuwa, mapigano makali yamejiri kati ya pande mbili ambapo karibu watu 120 wameuawa. Kwa mujibu wa afisa huyo wa serikali, watu 100 kati ya wahanga hao ni wapiganaji wa al-Huthi na kwamba 20 wengine ni askari wa serikali.
Hii ni katika hali ambayo Brigedia Jenerali Ahmad Ali al-Ashul, wa jeshi la Yemen, amezilaumu baadhi ya pande ambazo hakuzitaja, kwamba zinafanya njama kwa lengo la kuzusha vita vya ndani nchini Yemen na kusisitiza kuwa, njama hizo zitaambulia patupu. Wanachama wa al-Huthi wanaituhumu serikali ya Sanaa kuwa inayaunga mkono makundi ya kitakfiri huko kaskazini mwa nchi hiyo kwa lengo la kudhoofisha nafasi yao, sambamba na kuandaa mazingira ya kupenya matakfiri katika mkoa huo wa Imran wa kaskazini mwa Yemen.

No comments: