Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, June 8, 2014

Wanadiplomasia wa Iran, Marekani kukutana

Wanadiplomasia wa ngazi za juu wa Iran na Marekani wanatazamiwa kukutana wiki ijayo kabla ya duru mpya ya mazungumzo ya nyuklia kati ya Jamhuri ya Kiislamu na madola sita makubwa duniani.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa na kusema mkutano kuhusu jumbe za Iran na Marekani utafanyika Geneva kuanzia tarehe 9 hadi 10 Juni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi ataongoza ujumbe wa Iran katika mazungumzo hayo huku ujumbe wa Marekani ukiongozwa na Wendy Sherman Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani. Araqchi amesisitiza kuwa mkutano wake na Sherman utahusu kadhia ya nyuklia pekee. Mkutano huo unakuja kabla ya duru nyingine ya mazungumzo kuhusu mpango wa Iran wa nishati ya nyuklia ambayo yanatazamiwa kufanyika Juni 16-20 katika mji wa Vienna nchini Austria. Maafisa wa Iran pia wanatazamiwa kukutana na wanadiplomasia wa Russia huko Roma, Italia kati ya Juni 11 na 12. Aidha maafisa wa Iran wanatazamiwa pia kufanya mazungumzo na wawakilishi wengine wa kundi la 5+1 ambalo linajumuisha China, Russia, Ufaransa, Uingereza, Marekani na Ujerumani. Iran imekuwa ikifanya mazungumzo na madola hayo kwa lengo la kuondoa hitilafu zilizopo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran wenye malengo ya amani.

No comments: