Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, June 8, 2014

Yemen yataka Marekani isingilie mambo yake

Maafisa wa kijeshi nchini Yemen sasa wameitaka Marekani iache kuingilia mambo yake ya ndani. Wakizungumza Jumamosi, maafisa hao wa kijeshi wamesema Marekani inapaswa kusitisha oparesheni zake za ndege zisizo na rubani (drone) ambazo zinatekeleza mauaji nchini humo.  Aidha wamesema vikosi vya usalama vya Yemen ndivyo vyenye jukumu la kuwalinda Wayemen kutokana na hujuma za kigaidi na hivyo vikosi vya kigeni havipaswi kujihusisha na suala hilo.
Maafisa hao wameongeza kuwa Marekani imepelekea ugaidi kuongezeka Yemen kwa kutumia ndege zisizo na robani.
Mbali na Yemen, Marekani imekuwa ikitumia ndege hizo zisizo na rubani kushambulia maeneo mbalimbali ya nchi za Kiislamu za Somalia, Afghanistan, Syria na Pakistan kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Katika nchi hizo pia aghalabu ya wanaopoteza maisha katika hujuma za ndege hizo za Marekani ni raia wa kawaida wakiwemo wanawake na watoto wasio na hatia.

No comments: