Watu saba wameawa katika mapigano yaliyozuka kati ya waungaji
mkono na wafuasi wa Rais Muhammad Morsi hapo jana huko Cairo mji mkuu wa
Misri. Watu watatu waliuawa katika ghasia zilizojiri kati ya pande
mbili hizo kwenye maeneo tofauti ya Cairo.
Huku hayo yakiripotiwa wapinzani wa Morsi jana walichoma moto makao
makuu ya kundi la Ikhwanul Muslimin katika mji wa Hilwan wa kaskazini
mwa Misri.
Mapema hiyo jana pia jeshi la Misri liliandaa ramani ya njia
kwa lengo la kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo ambapo kwa mujibu
wa ramani hiyo ya njia, itabidi bunge livunjwe na katiba isimamishwe.
Wakati huo huo Rais Muhammad ameliomba jeshi la nchi hiyo kuondoa
muda wake liliouainisha kwa ajili ya kusimamisha katiba na kulivunja
bunge huku akiashiria juu ya uhalali wa kikatiba wa utawala wake.







No comments:
Post a Comment