Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, July 3, 2013

Jumatano, Julai 3, 2012

Leo ni Jumatano tarehe 24 Shaaban 1434 Hijria inayosadifiana na Julai 3, 2013.
Siku kama ya leo miaka 25 iliyopita ndege ya abiria aina ya Airbus ya shirika la ndege ya Iran iliyokuwa ikitoka Bandar Abbas kusini mwa Iran na kuelekea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu ilishambuliwa kwa makombora mawili kwenye maji ya Ghuba ya Uajemi. Manowari ya kijeshi ya Marekani USS Vincennes ilifyatua makombora hayo na kuua shahidi watu wote 298 waliokuwa katika ndege hiyo. Shambulio hilo lilidhihirisha zaidi unyama wa serikali ya Marekani. Viongozi wa Marekani walizidisha ukatili wao pale walipomzawadia medali ya ushujaa nahodha wa meli hiyo kutokana na kitendo hicho kilichoonekana na serikali ya Washington kuwa eti ni cha kishujaa.

Siku kama ya leo miaka 43 iliyopita, inayosadifiana na 12 Tir 1349 Hijria Shamsia, alifariki dunia Allamah Abdul Hussein Amini, faqihi mkubwa na mwandishi hodari wa Kiislamu. Kitabu cha kwanza cha mwanazuoni huo alikipa jina la Shuhadaul Fadhila. Hata hivyo kitabu mashuhuri na kikubwa zaidi cha Allamah Amini ni kile cha "al Ghadiir Fil Kitab Wassunah" ambamo ndani yake amekosoa na kuchunguza vitabu vikubwa na marejeo vya Kiislamu 150  akithibitisha wilaya na haki ya Imam Ali bin Abi Twalib ya kuwa Khalifa na Imam wa Waislamu baada ya Mtume Muhammad (saw). Mwanachuoni huyo alisafiri kwa taabu katika nchi za India, Uturuki, Syria, Misri na Iraq kwa ajili ya kukusanya ushahidi mbalimbali wa kihistoria alioutumia katika kitabu hicho.
Na siku kama ya leo miaka 109 iliyopita inayosadifiana na 3 Julai 1904, alifariki dunia Theodor Herzl mwasisi wa harakati ya Kizayuni. Herzl alizaliwa mwaka 1860 mjini Bucharest mji mkuu wa Hungary na kisha kuelekea Austria. Mnamo mwaka 1897, aliasisi Taasisi ya Kimataifa ya Kizayuni kwenye kongamano lililofanyika nchini Uswisi. Herzl alifariki mwaka 1904, huku akiwa ameacha mikakati ya kuasisiwa utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel, kwenye ardhi za Palestina utawala ambao hadi leo unaendelea kufanya jinai kubwa na kusababisha maafa yasiyo na kifani dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina.

No comments: