Chama cha Kongresi ya Kitaifa cha Sudan kimeitaka jamii ya kimataifa
ifanye juhudi za kufutiwa vikwazo nchi hiyo. Al-Haj Adam Youseff, Makamu
Mwenyekiti wa chama cha National Congress Party (NCP) kinachotawala
nchini Sudan ameitaka jamii ya kimataifa iiondoleee vikwazo Sudan na
hivyo kuisaidia katika uwanja wa ustawi na maendeleo. Kiongozi huyo
mwandamizi wa chama tawala nchini Sudan amesema kuwa, licha ya kuweko
mzingiro na njama za maadui za kuusambaratisha uchumi wa nchi hiyo,
lakini katika kipindi cha miaka 24 iliyopita Khartoum imeweza kupiga
hatua muhimu za kimaendeleo.
Makamu Mwenyekiti wa chama tawala nchini
Sudan cha National Congress Party (NCP) ameyataka makundi yote ya
kisiasa nchini humo kujiunga na hati ya makubaliano ya amani na hivyo
kusaidia juhudi za kurejesha amani na utulivu katika nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment