Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, July 2, 2013

Jumanne, Julai 02, 2013

Leo ni Jumanne tarehe 23 Shaaban 1434 Hijria sawa na tarehe 2 Julai 2013.
Siku kama ya leo miaka 124 iliyopita mfumo wa kisultani ulifutwa huko Brazil na badala yake ukaasisiwa mfumo wa jamhuri bila ya umwagaji damu wowote na katika hali ya utulivu. Mfalme wa mwisho wa Brazil alikuwa Pedro wa Pili ambaye alifanya jitihada za kufanya mabadiliko nchini humo. Hatua za mfalme huyo hususan ile ya kuondoa biashara ya utumwa mwaka 1888, iliwakasirisha wamiliki waliokuwa wakiunga mkono mfumo wake wa kisultani. Pedro wa Pili alienguliwa madarakani bila ya mapambano yoyote na mfumo wa jamhuri ukaasisiwa nchini Brazil.

Miaka 88 iliyopita katika siku kama hii ya leo alizaliwa Patrice Lumumba mwasisi wa Kongo. Lumumba alitoa mchango mkubwa katika juhudi za kukombolewa Kongo wakati wa harakati za ukombozi wa nchi za Kiafrika. Lumumba aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi baada ya kuundwa Jamhuri ya Kongo mwaka 1960. Patrice Lumumba aliuawa mwaka 1961 na vibaraka wa Marekani na Ubelgiji baada ya kuvumilia mateso na unyama mkubwa. Patrice Lumumba aliandika vitabu kadhaa wakati wa uhai wake na mashuhuri zaidi ni kile alichokita" Kongo, Nchi Yangu."
Na tarehe 11 Tir miaka 31 iliyopita Ayatullah Muhamad Saduqi alimu mkubwa, mwanamapambano na Imamu wa Ijumaa wa mji wa Yazd huko katikati mwa Iran, aliuawa shahidi na vibaraka wa kundi la kigaidi la Munafiqiin na kuwa shahidi wa nne aliyeuawa katika mihrabu ya swala katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Ayatullah Muhamad Saduqi alikamilisha masomo yake ya kidini katika Hauza ya mji mtakatifu wa Qum Iran na kustafidi na bahari kubwa ya elimu kutoka kwa walimu mashuhuri wa kituo hicho cha kielimu kama vile Ayatullah Burujerdi na Ayatullah Khansari.

No comments: