Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, July 2, 2013

Rais Barack Obama aitembelea Tanzania

Rais Obama wa Marekani amewasili leo nchini Tanzania ikiwa ni nchi ya mwisho kuitembelea katika safari yake ya kuzitembelea nchi za eneo la Kuisni mwa Jangwa la Sahara.
Obama amelakiwa mjini Dar es salaam na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na umati mkubwa wa watu waliokuwa wakicheza, kupiga vigelegele na kupeperusha bendera za nchi hizo mbili.

Hii ni ziara ya pili ya Rais wa Obama Barani Afrika na anaitembelea Tanzania baada ya ziara ya Rais Xi Jimping wa China aliyeitembelea nchi hiyo Machi 28 mwaka huu. Miongoni mwa sababu zinazoelezwa za safari ya Obama nchini Tanzania ni nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi 10 duniani ambazo uchumi wake unakua kwa kasi.

No comments: