Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail
Showing posts with label Wasomali na Waithiopia 259 wakimbilia magharibi mwa Yemen. Show all posts
Showing posts with label Wasomali na Waithiopia 259 wakimbilia magharibi mwa Yemen. Show all posts

Tuesday, May 15, 2012

Wasomali na Waithiopia 259 wakimbilia magharibi mwa Yemen

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Yemen imeripoti kuwa, watu 259 wamekimbilia katika fukwe za magharibi za nchi hiyo kutokea barani Afrika.
Wizara hiyo imeongeza kuwa, wakimbizi hao wamewekwa katika kambi maalumu za wakimbizi nchini Yemen.
Taarifa ya wizara hiyo imeongeza kuwa, watu hao wametokea eneo la Pembe ya Afrika na wamekimbilia kwenye fukwe za mikoa miwili ya Taiz na Hadhramaut nchini Yemen. Wanawake 58 na watoto wadogo 14 ni miongoni mwa wakimbizi hao 259.