Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail
Showing posts with label Umoja wa Waislamu ndio ufunguo wa mafanikio yao. Show all posts
Showing posts with label Umoja wa Waislamu ndio ufunguo wa mafanikio yao. Show all posts

Saturday, January 26, 2013

Umoja wa Waislamu ndio ufunguo wa mafanikio yao .

Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, umoja wa Waislamu ndio utakaokuwa chimbuko la ushindi wao dhidi ya njama mbalimbali za uistikbari na maadui. Ayatullah Muhammad Kashani pia ametoa mkono wa baraka kwa kuwadia maadhimisho ya kuzaliwa mbora wa viumbe Mtukufu Mtume wa Uislamu Muhammad al Mustafa (SAW), na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa mjukuu wa mtukufu huyo Imam Jaafar Swadiq (as) na kuanza kwa Wiki ya Umoja. Amesema kuwa, Wiki ya Umoja ni fursa muhimu ya kuimarisha umoja kati ya Waislamu wote kwa ujumla na kwamba, mambo hayo ndiyo yatakayoweza kuzishinda njama za maadui.