Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, June 8, 2014

Kaburi la umati katika Kanisa Katoliki Ireland

Kanisa Katoliki duniani linakabiliwa na mashinikizo makali kuhusu udhalilishaji wa watoto wadogo baada ya mtafiti kugundua mafuvu na mifupa ya watoto taribani 800 wakiwa wamezikwa katika kaburi la umati nchini Ireland.
Serikali ya Ireland imetangaza kuwa inatafakari kufanya uchunguzi rasmi baada ya utafiti mpya kubaini kupata rekodi za watoto 796 waliopoteza maisha na kuzikwa katika makaburi yasiyo na alama huko magharibi mwa nchi.

Watoto hao walirundikwa katika kaburi la umati lililo karibu na nyumba ya mayatima iliyokuwa ikisimamiwa na watawa wa kike katika eneo la Tuam, Kaunti ya Galway. Mayatima hao walikuwa wale waliozaliwa nje ya ndoa. Watoto hao ambao baadhi walikuwa na umri wa siku mbili walipoteza maisha kati ya mwaka 1924 hadi 1961. Rekodi zinaonyesha kuwa walipoteza maisha kutokana na lishe duni, magonjwa na maradhi, ulemavu na kuzaliwa kabla ya wakati. Uchunguzi unaonyesha kuwa watoto hao walitupwa katika eneo lilokuwa na dimbwi la maji machafu. Dimbwi hilo liligeuzwa kuwa kaburi la umati. Mashirika ya kutetea haki za binaadamu yamelitupia lawama Kanisa Katoliki na kusema lilihusika na mauaji hayo ya umati. Kanisa Katoliki Ireland limedai kuwa halina habari kuwa eneo hilo lilikuwa kaburi la umati. Katika miaka ya hivi karibuni Kanisa Katoliki limekuwa likilaumiwa vikali kwa kuwadhalilisha kijinsia watoto walio chini ya usimamizi wake.

No comments: