Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 23, 2014

Waasi nchini Mali: Tumeua askari wengi wa serikali

Duru za habari nchini Mali zinaeleza kuwa, jeshi la serikali ya nchi hiyo limepata hasara kubwa katika mapambano yake na wanamgambo wa kaskazini mwa nchi hiyo. Msemaji wa kundi la waasi wa Tuareg maarufu kwa jina la 'Harakati ya Ukombozi wa Azawad,' Ag At'har amesema kuwa, wapiganaji wa kundi hilo wamewaua askari 40 wa serikali ya Mali na kujeruhi wengine 50 katika mapigano ya hivi karibuni, kaskazini mwa nchi hiyo. Msemaji wa harakati hiyo ambaye anaishi huko Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, amedai kuwa ni wanamgambo wawili tu ndio waliouawa katika mapigano hayo na kuongeza kuwa, mbali na askari 40 kuuawa, askari wengine 70 wa serikali wametekwa na wapiganaji hao.
Hii ni katika hali ambayo hapo juzi askari mmoja wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa mataifa nchini Mali, alithibitisha kutokea hasara kubwa kwa askari wa serikali ya Bamako katika vita vyake huko kaskazini mwa Mali. Tangu siku ya Jumamosi iliyopita, mji wa Kidal, umekuwa ukishuhudia wimbi la mapigano ya hapa na pale kati ya pande mbili. Weledi wa mambo wanailaumu Ufaransa kwa kuhusika na mapigano hayo, ambayo ni njia moja wapo ya kutaka kuendelea kubakisha askari wake ndani ya ardhi ya nchi hiyo.

No comments: