Ethiopia imemuita balozi wa Misri mjini Addis Ababa na kutaka maelezo
kuhusiana na matamshi inayodai kuwa ya kiadui yaliyotolewa na wanasiasa
wa Misri kuhusu ujenzi wa bwawa la Ethiopia katika Mto Nile. Dina Mufti
msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ethiopia amesema, Tarek Ghoneim
Balozi wa Misri mjini Addis Ababa ameitwa ili aeleze juu ya matamshi
hayo ya kiadui. Mwanzoni mwa wiki hii wanasiasa wa Misri
walitahadharisha juu ya kupunguzwa fungu la maji la Misri katika Mto
Nile, huku wakipendekeza mpango wa kuhujumu au kuwasaidia waasi dhidi ya
serikali ya Addis Ababa ambayo imeanza ujenzi wa bwawa kubwa katika
Blue Nile wiki iliyopita ili kuzalisha umeme. Pia Waziri wa Mambo ya Nje
wa Misri Mohammed Kamel Amr jana alisema kwamba, usalama wa maji wa
nchi yake hauwezi kupuuzwa na kutoa wito wa kutafutwa suluhisho la amani
la suala hilo na nchi jirani za Sudan na Ethiopia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment