Kufuatia kuongezeka ukosoaji mkubwa wa kila siku juu ya kuongezwa muda
wa shughuli zake hadi mwezi Disemba mwaka huu, hatimaye Kongresi ya
Taifa nchini Libya yaani bunge, limetangaza kuwa, uchaguzi wa bunge
utafanyika tarehe 25 mwezi ujao. Hayo yamesemwa na Naibu wa pili wa
Spika wa bunge la nchi hiyo, bwana Swaleh al-Makhzum na kuongeza kuwa,
tarehe 25 Juni itakuwa siku ya kihistoria kwa Walibya. Kwa utaratibu huo
Kongresi ya Taifa ya Libya imemaliza kigugumizi kuhusiana na suala zima
la uchaguzi huo.
Hii ni katika hali ambayo machafuko ya kila mara
ambayo yanaendelea nchini humo, yamezua maswali mengi kuhusu uwezekano
wa kufanyika uchaguzi huo. Wakati huo huo Jenerali mstaafu wa nchi hiyo,
Khalifa Haftar ameituhumu serikali ya mpito ya Tripoli kwamba
inawaunga mkono magaidi na kusema kuwa, mapigano dhidi ya wanamgambo
wenye silaha yataendelea. Zaidi ya hayo, Muhammad Hijazi, kamanda mkuu
wa jeshi la Libya amesema kuwa, jeshi la taifa limejiandaa vilivyo
kuendelea na vita dhidi ya makundi yenye misimamo ya kufurutu ada,
magaidi na waungaji wao mkono nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment