Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watu wasiopungua 181 waliuawa, 217
kujeruhiwa na wengine 52 elfu kuwa wakimbizi, kwenye mapigano ya
kikabila yaliyotokea nchini Kenya.
Ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA
imeeleza kuwa, takwimu za mauaji, majeruhi na wakimbizi hao ni za
kutokea mwezi Januari mwaka huu hadi sasa.
Msemaji wa OCHA katika
Ukanda wa Afrika Mashariki Matthew Conway amesema kuwa, serikali ya
Kenya kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu la nchi hiyo,
asasi zisizo za kiserikali pamoja na mashirika mengine ya kimataifa
yametoa misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi na majeruhi wa mapigano hayo
ya kikabila. Conway ameongeza kuwa, mikoa ya Rift Valley, Magharibi na
Kaskazini Mashariki mwa Kenya ndio iliyoathirika sana na mapigano hayo
ya kikabila.
Taarifa ya OCHA imeeleza kuwa, wahanga wengi wa mapigano hayo ni
kutoka maeneo ya kaskazini mwa Kenya, ambayo yalikubwa na mapigano
makubwa kati ya makabila ya Garre na Degodia na kusababisha mauaji ya
watu wasiopungua 70.







No comments:
Post a Comment