Kwa akali watu watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, baada ya
bomu la kutegwa garini lililoulenga msafara wa vikosi vya kulinda amani
vya Umoja wa Afrika AMISOM kulipuka mjini Mogadishu.
Hili linahesabiwa kuwa shambulio jipya dhidi ya vikosi vya AMISOM
katika barabara yenye msongamano mkubwa wa watu pambizoni kidogo mwa mji
wa Mogadishu. Duru za habari zinasema kuwa, baada ya kutokea mlipuko
huo, zilisikika sauti za silaha nzito katika eneo hilo.
Naibu Meya wa
Mogadishu ameviambia vyombo vya habari kwamba watu watatu akiwemo
mtegaji wa shambulio hilo, wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.
Naibu Meya wa Mogadishu ameongeza kuwa, hakuna hata askari mmoja wa
AMISOM aliyeuawa au kujeruhiwa kwenye shambulio hilo.
Hadi sasa hakuna kundi lolote lililojitangaza kuhusika na shambulio
hilo lililofanyika leo, lakini kundi la al Shabab limekuwa likijitangaza
kuhusika na mashambulio kama hayo dhidi ya vikosi vya kulinda amani vya
Umoja wa Afrika nchini Somalia.







No comments:
Post a Comment