Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, July 13, 2013

Obasanjo mwangalizi mkuu wa uchaguzi Zimbabwe

Olusegun Obasanjo Rais wa zamani wa Nigeria ameteuliwa na Umoja wa Afrika kuwa mkuu wa jopo la waangalizi wa uchaguzi  mkuu nchini Zimbabwe. Taarifa zinasema kuwa, Umoja wa Afrika umeeleza kuwa, taasisi na asasi nyingine zisizokuwa za kiserikali na wajumbe kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Ustawi ya Kusini mwa Afrika SADC watakuwa miongoni mwa waangalizi wa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 31 mwezi huu.
Uchaguzi huo unafanyika katika hali ambayo, Morgan Tsvangirai Waziri Mkuu wa Zimbabwe na kiongozi wa chama cha MDC anadai kuwa, vyombo vya kupasha habari, kikosi cha usalama na jeshi la polisi hivyo vyote bado vinadhibitiwa na Rais Mugabe wa nchi  hiyo. Wakati huohuo, Umoja wa Ulaya umetangaza uwezekano wa kuondolewa  vikwazo dhidi ya Zimbabwe iwapo uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki. Roland van de Geer Balozi wa Umoja wa Ulaya amesema nchini Afrika Kusini kwamba, iwapo waangalizi wa kieneo watathibitisha kuwa uchaguzi huo ulifanyika bila ya mizengwe yoyote, umoja huo utaondoa vikwazo dhidi ya serikali ya Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo.

No comments: