Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, July 13, 2013

Jumamosi, Julai 13, 2013

Leo ni Jumamosi tarehe 4 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka 1434 Hijiria mwafaka na tarehe 13 Julai mwaka 2013 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 64 iliyopita, moto mkubwa ulitokea huko Roma mji mkuu wa utawala wa kifalme wa Rumi. Sehemu kubwa ya mji wa kihistoria na mkongwe wa Roma iliungua na wakazi wengi wa mji huo walipoteza maisha yao kutokana na moto huo.
Moto huo ulikuwa kisingizio tosha kwa Nuren mtawala mmwagadamu wa Kirumi ambaye aliwauwa kwa umati watu zaidi ya laki moja na baadaye kuwatuhumu Wakristo kuwa ndio walioanzisha moto huo.
Miaka 858 iliyopita yaani tarehe 4 Ramadhani mwaka 576 Hijria, alifariki dunia, Muhammad bin Muhammad mashuhuri kwa jina la Ibnu Khorasani. Ibnu Khorasani alikuwa mshairi, mwandishi na mtaalamu wa elimu ya Nahw. Alizaliwa mwaka 494 Hijria huko Khorasan kaskazini mashariki mwa Iran. Akiwa na lengo la kutafuta elimu, Muhammad bin Muhammad alielekea katika mji wa Baghdad nchini Iraq. Kutokana na kipaji alichonacho, alimu huyu alifanikiwa kuzikwea haraka haraka daraja za kielimu na kuondokea kuwa alimu mkubwa na mtajika.
Siku kama ya leo miaka 242 iliyopita, baharia na nahodha mashuhuri wa Kiingereza aliyejulikana kwa jina la James Cook alikamilisha safari yake ya kitafiti na kielimu ya kuelekea The Great Southern Continent. Safari hiyo ilikuwa imeanza tarehe 26 Julai mwaka 1768. Safari hiyo ndefu iliishirikisha pia timu ya watalaamu wa elimu ya Sayansi Asilia au Natural Science kwa kimombo. Wataalamu hao walikuwa na nia ya kufanya utafiti wa kielimu kuhusiana na mimea pamoja na viumbe wanaopatikana katika maeneo hayo.

No comments: