Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, July 13, 2013

Malema aanzisha chama cha kisiasa A. Kusini

Julius Sello Malema mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Vijana ya chama tawala cha African National Congress (ANC) nchini Afrika Kusini ameanzisha chama cha kisiasa kwa shabaha ya kupambana na chama tawala.
Malema ambaye alikuwa kiongozi mwenye ushawishi ndani ya chama cha ANC na hasa kwa matabaka ya vijana, alitimuliwa ndani ya  chama cha ANC mwezi Februari mwaka huu kwa tuhuma za ufisadi na ubadhirifu wa mali za chama.
Malema ameunda chama chake cha Economic Freedom Fighters (EFF) chenye lengo la kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi nchini humo. Chama hicho chenye kufuata mrengo wa kushoto, kitajikita zaidi katika kupambana na vitendo vya uporaji wa ardhi na suala la ubinafsishwaji sekta ya madini nchini Afrika Kusini.
Julius Malema amesisitiza kuwa, yuko tayari kushiriki kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwaka ujao nchini humo.

No comments: