Waziri wa Utamaduni na Habari wa Sudan, ameyataja mashambulizi ya
makundi ya waasi nchini humo, kuwa yanayofanyika kwa njama za Wazayuni
kwa minajili ya kuutokomeza umoja wa kitaifa na kuigawa nchi. Ahmad
Bilal Othman ameyasema hayo kupitia redio ya Sudan na kufafanua kuwa,
mashambulizi ya waasi nchini humo, yanafanyika kwa njama kamili za
Wazayuni kwa lengo la kuharibu umoja na mshikamano, kuvuruga usalama na
uthabiti wa Sudan, huku lengo kuu likiwa ni kuigawa nchi hiyo.
Amesisitizia juu ya umuhimu wa kukabiliana na njama hizo za Israel dhidi
ya Sudan. Hii ni katika hali ambayo kuna uwezekano serikali ya Khartoum
ikakataa kufanya mazungumzo na waasi, baada ya waasi hao kutekeleza
jinai mbalimbali dhidi ya wakazi wa Kordofan na Blue Nile katika siku za
hivi karibuni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment