Jeshi la Iraq limetangaza kuwa, limefanikiwa kuwatia mbaroni magaidi 11
ambao walikuwa wakitafutwa kwa muda mrefu, kwa kuhusika na vitendo vya
kigaidi huko kaskazini mwa nchi hiyo. Jeshi la usalama limetangaza kuwa,
magaidi hao walitiwa mbaroni katika oparesheni kali iliyofanyika mjini
Mosul katikati ya mkoa wa Nainawah kaskazini mwa Iraq. Limeongeza kuwa,
mbali na magaidi hao, jeshi pia limefanikiwa kudhibiti silaha na zana
nyingine za kijeshi za magaidi hao. Aidha hapo jana vilifanikiwa
kugundua gari lililokuwa limetegwa bomu tayari kulipuliwa huko kusini
mwa mji wa Mosul na kumtia mbaroni mtu mmoja. Wakati huo huo raia 14
waliuawa na kujeruhiwa hapo jana katika miripuko miwili iliyotokea
katika eneo la Nahrawan mjini Baghdad. Kabla ya hapo pia mabasi mawili
ya wafanyaziara wa Kiirani yalilipuliwa kwa mabomu nchini humo na
kusababisha mauaji na majeruhi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment